karibu kituo cha nishati ngarenanyuki

MAELEZO ZAIDI YA MITAMBO YA BIOGESI


MUHIMU:Unaweza kuchagua ukubwa wa mtambo wa nishati ya gesi kutegemea idadi ya mifugo uliyonayo na mahitaji yako ya nishati.

Ukubwa wa Mtambo
Idadi ya Ng’ombe
Masaa ya kupika kwa siku:

Ukubwa wa Mtambo
Idadi ya Ng’ombe
Masaa ya kupika kwa siku
4m3
2 → 3
2→ 4
6m3
4→ 5
4→ 6
9m3
5→ 7
6→ 10
13m3
10→15
8→15

Idadi iliyoonyeshwa ni ya ng’ombe wanaolishwa kwenye zizi muda wote ambapo kinyesi hupatikana kutoka kwenye zizi. 
Kama ng’ombe hupelekwa malishoni wakati wa mchana na kurudi kwenye zizi wakati wa usiku, inatakiwa kupatikana kinyesi sawa na ng’ombe wasio chungwa ili kupata kiasi cha gesi kinacholingana na mahitaji yako. 

JE, UNAHITAJI NINI KUWA NA MTAMBO WA NISHATI YA GESI?

1) Unahitaji kuwa na angalau ng’ombe wawili wa kudumu karibu na mtambo. 

2) Ng’ombe wako wawepo muda wote katika mwaka. Unatakiwa kulisha mtambo hata wakati wa ukame.

3) Hakikisha kuwa utaweza kulisha ng’ombe wakati wa ukame.

4) Hakikisha kuwa na maji wakati wote wa mwaka 

5) Utahitaji kulisha mtambo angalao mara moja kwa siku. 


Home page: nyumbani