karibu kituo cha nishati ngarenanyuki

Tuesday, February 8, 2011

KITUO CHA NISHATI


Mafundi wote wa umemejua, ambao wanafanya kazi pamoja na Kituo cha Nishati cha Jamii, wamepata mafunzo ya kutosha, na wana uzoefu mkbubwa wa kiufundi.

Mhudumu wa kituo anapatikana kituoni kila siku za jumatatu hadi jumamosi kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11: 00 jioni.
Kwa mawasiliano zaidi kuhusu umemejua piga za simu  kwa namba zifuatazo: (contact)
MRADI WA NISHATI
MBADALA (BEST RAY)
Mradi huu umefadhiliwa na Kamisheni Ya Jumuia Ya Ulaya (NI programu ya 9 ya nishati ya Jumuia ya Ulaya kwa Tanzania) na untekelezwa na Istituto Oikos. picha zaidi:bonyeza

Tuesday, January 25, 2011

MITAMBO YA NISHATI YA BIOGAS

 MTAMBO WA NISHATI YA GESI (BIOGAS) NI CHAGUO LA KISASA:

Unaweza kujenga mtambo wa nishati ya gesi kama unafuga ng’ombe na una uhakika wa kupata maji na kinyesi cha kutosha.

Mtambo wa Nishati ya Gesi unaweza kutengeneza takriban gesi ya kupikia kwa masaa mawili hadi nane kwa siku kutegemea ukubwa wa mtambo na kiasi cha malighafi inayotumika.






A) sehemu ya kuchanganyia kinyesi cha mifugo, mkojo au maji kwa kipimo cha ndoo moja ya kinyesi kwa kila ndoo moja ya maji

B) shimo kuu la kuchachulia na kuhifadhia gesi.

C) Chemba Mtanuko

D) sehemu ya kutolea tope chujio (slurry)




Kwa maelezo zaidi(bonyeza)

Tuesday, January 18, 2011

GHARAMA YA UJENZI WA MTAMBO WA NISHATI

Gharama ya ujenzi wa mtambo wa nishati ya gesi huanzia Shilingi Milioni 1 kwa mtambo mdogo. Gharama huongezeka kutegemea ukubwa wa mtambo, upatikanaji wa vifaa na usafiri.
Inaonyesha kuwa gharama ya T. Shs 1.4 Milioni kwa kujengewa mtambo wa biogas wa ujazo wa 6m3 ni kubwa. Gharama hiyo ni sawa na kulipa Shilingi 15,000/- kwa mwezi kwa matumizi ya nishati ya kupikia. Mwenye mtambo huo atatumia nishati hiyo bure baada ya miaka nane.
Wasiliana na Vituo vya Nishati na Mafundi kwenye jamii yako kupata bei kamili. Waulize kama Camartec au Oikos wanatoa ruzuku na watembelee ili kuhakiki.