karibu kituo cha nishati ngarenanyuki

Tuesday, January 18, 2011

GHARAMA YA UJENZI WA MTAMBO WA NISHATI

Gharama ya ujenzi wa mtambo wa nishati ya gesi huanzia Shilingi Milioni 1 kwa mtambo mdogo. Gharama huongezeka kutegemea ukubwa wa mtambo, upatikanaji wa vifaa na usafiri.
Inaonyesha kuwa gharama ya T. Shs 1.4 Milioni kwa kujengewa mtambo wa biogas wa ujazo wa 6m3 ni kubwa. Gharama hiyo ni sawa na kulipa Shilingi 15,000/- kwa mwezi kwa matumizi ya nishati ya kupikia. Mwenye mtambo huo atatumia nishati hiyo bure baada ya miaka nane.
Wasiliana na Vituo vya Nishati na Mafundi kwenye jamii yako kupata bei kamili. Waulize kama Camartec au Oikos wanatoa ruzuku na watembelee ili kuhakiki.